Pata muhtasari wa vyuo vya ualimu diploma Dar es Salaam—serikali na binafsi—pamoja na kozi zinazopatikana mtandaoni, nyaraka za kupakua, maoni ya wanafunzi na taarifa za private colleges.
Faida za Kusoma Dar es Salaam Tofauti na Mikoani
- Fursa nyingi za mazoezi na ajira.
- Upatikanaji mpana wa kozi na vyuo.
- Miundombinu bora ya kujifunzia.
- Mtandao mpana wa watu (networking).
- Upatikanaji rahisi wa huduma muhimu.
- Fursa za kujifunza mambo mapya nje ya darasa.
- Urahisi wa kupata taarifa mpya
Orodha Kamili ya Vyuo Vya Diploma ualimu Dar Es Salaam
| Jina la Chuo | Wilaya / Halmashauri | Umiliki | Ngazi Zinatolewa |
|---|---|---|---|
| Dar es Salaam Mlimani Teachers College | Binafsi | Cheti, Diploma | |
| West Dar es Salaam Teachers College | Binafsi | Cheti, Diploma | |
| Joshua Teachers Training College | Binafsi | Cheti, Diploma | |
| Arafah Teachers College | Ilala MC | Binafsi | Cheti, Diploma |
| Montessori Teachers Training College | Temeke MC | Binafsi | Cheti, Diploma |
| Capital Teachers College | Kinondoni MC | Binafsi | Cheti, Diploma |
| Arizona Teachers College | Ilala MC | Binafsi | Cheti, Diploma |
| Kirinjiko Islamic Teachers College | Temeke MC | Binafsi | Cheti, Diploma |
| Kindercare Teachers College | Kinondoni DC | Binafsi | Cheti, Diploma |
Mambo Ya Kuzingatia Kabla Hujajiunga Na Vyuo Vya Ualimu
Mambo ya Kuzingatia Kabla ya Kujiunga na Chuo cha Ualimu
-
Uhalali wa Chuo (Registration & Accreditation)
Hakikisha kimesajiliwa na NACTVET au TCU kulingana na ngazi ya masomo. -
Ngazi ya Mafunzo Wanazotoa (Cheti / Diploma / Degree)
Chagua chuo kinachotoa ngazi unayotaka na kinachoendana na malengo yako. -
Mtaala na Ubora wa Mafunzo
Angalia kama mtaala unafuata viwango vya Wizara ya Elimu na unaendana na mahitaji ya ufundishaji wa sasa. -
Ukubwa na Uwezo wa Mazingira ya Kujifunzia
Vyumba vya madarasa, maabara ya TEHAMA, vitabu, maktaba, hostel, n.k. -
Ada na Gharama Zingine
Lingaisha ada ya masomo, gharama za hostel, chakula, na vifaa vya kujifunzia. -
Ajira na Soko la Walimu
Angalia historia ya wahitimu wa chuo hicho kupata ajira au kuendelea na masomo. -
Mahali (Location) na Usalama
Chagua eneo salama na linalokuwezesha kusoma kwa amani. -
Sifa za Kujiunga (Entry Requirements)
Hakikisha ufaulu wako unakidhi viwango vya kuingia kwenye Cheti/Diploma ya Ualimu.
Hatua Za Kujiunga Na Vyuo Vya Ualimu
-
Tambua chuo unachotaka kujiunga nacho
Chagua chuo kilichosajiliwa na kinachotoa kozi unayoitafuta (Cheti/Diploma). -
Angalia sifa za kujiunga (Entry Requirements)
Hakikisha ufaulu wa mitihani yako unakidhi vigezo vya kozi. -
Jaza fomu ya maombi (Online au Ofisini)
Ingia kwenye tovuti ya chuo au NACTVET CADS kama chuo kinatumia mfumo wa kitaifa. -
Wasilisha nyaraka muhimu
Vyeti vya elimu, picha, kitambulisho, na risiti ya malipo ya ada ya maombi. -
Subiri majibu ya udahili na thibitisha nafasi
Ukipokea “Admission Letter,” lipia ada ya uthibitisho na ujiandae kuanza masomo.