Taratibu Za Uhamisho Wa Wanafunzi Shule za msingi, Sekondari na Vyuo

maombi ya uhamisho nacte

Zimetangazwa na kuendelea kutekelezwa taratibu za uhamisho wa wanafunzi kupitia mifumo rasmi ya serikali, ambapo wazazi na wanafunzi wanaweza kufanya tamisemi uhamisho wanafunzi kwa urahisi zaidi. Kupitia tamisemi uhamisho wanafunzi online, maombi mengi sasa yanafanyika kidigitali, yakirahisisha mchakato wa uhamisho wa wanafunzi tamisemi kuanzia ngazi ya shule ya msingi hadi sekondari na vyuo vya kati.

Katika makala hii, utapata mwongozo kamili wa taratibu za uhamisho wa wanafunzi, ikiwemo uhamisho wa wanafunzi shule ya msingi, uhamisho wa wanafunzi kidato cha kwanza, uhamisho wa wanafunzi kidato cha tatu na uhamisho wa wanafunzi kidato cha tano. Pia tutakueleza kuhusu maombi ya uhamisho wa wanafunzi yanayo endelea, namna ya kupata uhamisho wa wanafunzi sekondari pdf na mfumo wa uhamisho wa wanafunzi pdf, pamoja na taarifa muhimu kuhusu uhamisho wa wanafunzi NACTE na uhamisho wa wanafunzi vyuo vya kati ili kukusaidia kufanya maamuzi sahihi kwa urahisi.

Maombi ya Uhamisho wa Wanafunzi Wanaoendelea

Tafadhali soma kwa makini taarifa na mahitaji muhimu ya kuhama kabla hujaanza kufanya maombi ya uhamisho.

Masharti na Sifa kwa Waombaji

  1. Mwanafunzi anashauriwa kuhakiki na kufahamu taarifa za msingi za chuo anachotaka kuhamia kama vile, mahali chuo kilipo, hali ya hewa, ada na michango mingine. Kwa taarifa zaidi awasiliane na chuo anachotaka kuhamia.
  2. Uhamisho unawahusu wanafunzi waliopo katika mwaka wa masomo unaofuata kwa mkupuo wa MACHI na husika kwa mkupuo wa SEPTEMBA, ili kuhakiki kama upo katika mwaka husika bofya Hapa
  3. Mwanafunzi ataruhusiwa kuhama chuo kimoja kwenda kingine chenye kozi inayofanana
  4. Mwanafunzi ambaye hajafaulu au kuwa na mtihani wa marudio hahusiki na uhamisho huu
  5. Uhamisho utakubalika pale tu chuo unachotoka na unachotaka kuhamia vimeridhia
  6. Tarehe ya mwisho ya kuomba uhamisho ni inategemea na mwaka husika

Malipo ya Gharama ya uhamisho wa vyuo

  • Gharama za mchakato wa uhamisho ni Tsh 20,000/=, Malipo yaliyopokelewa hayatarejeshwa.
  • Bonyeza hapa kuendelea na malipo

maombi ya uhamisho nacte

Maombi ya Uhamisho Wa Wanafunzi Wa Sekondari

  1. Mzazi atatakiwa kuandika barua ya maombi ya kuhamisha mwanafunzi kwa Katibu Tawala wa Mkoa kwa kuzingatia mambo muhimu yafuatayo:
  2. Barua ya maombi ipitie kwa Mkuu wa Shule anayotarajia kuhamia Mwanafunzi mzazi akiomba nafasi katika shule hiyo
  3. Barua ya maombi pia ipitie kwa Mkuu wa Shule anakotoka mwanafunzi. Pia mzazi apeleke picha (passport size) nane kwa Mkuu wa Shule hiyo
  4. Barua hiyo hiyo ya maombi pia ipitie kwa Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya atokako mwanafunzi
  5. Baada ya Barua hiyo ya maombi kupitia ngazi hizo zote mwisho iletwe kwa Katibu Tawala wa Mkoa (Afisa Elimu wa Mkoa)
  6. Kama barua hiyo itapitishwa na Afisa Elimu wa Mkoa, Mzazi atapewa Barua ya uthibitisho wa kuhama nakala mbili ambazo ataziwasilisha moja kwa Mkuu wa Shule atokako na shule aendako kwa ajili ya kufungashiwa TSM9
  7. Taratibu wa uhamisho utakuwa umekamilika

Uhamisho Sekondari

Maombi Ya uhamisho Shule Za Msingi

  1. Mzazi/ Mlezi aandike barua kwenda katibu mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi (WEST) akifafanua ombi lake kwa kutoa sababu za msingi kuhusu uhamisho huo. Barua hiyo iwe ni ya kupitia kwa mwalimu mkuu, Afisa Elimu wilaya na Afisa Elimu wa mkoa husika.
  2.  Vitambulisho vya barua viwe:-
    1. Kadi ya Maendeleo ya mwanafunzi wa Elimu ya Msingi anaeingia Nchini.
    2. Barua iwe na picha ya mwanafunzi
  3. Afisa wa Wizara anayehusika atamwandikia barua ya kumtambulisha nchi anakokwenda.

uhamisho shule za msingi

Kwa kuhitimisha, ni muhimu kufuata taratibu zote za uhamisho wa wanafunzi kwa usahihi ili kuepuka usumbufu au kuchelewa kwa maombi. Hakikisha taarifa zote zinazojazwa kwenye mfumo ni sahihi, nyaraka muhimu zimekamilika, na maombi yanatumwa ndani ya muda uliopangwa. Kufuatilia taarifa kupitia mfumo rasmi wa Tamisemi kutasaidia kuongeza nafasi ya maombi yako kukubaliwa kwa haraka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *